Ahlul Bayt: Ni Nani, Si Nani

Front Cover
Ahlul Bayt Centre

Hiki ni cha pili katika mfululizo wa vitabu vilivyokusudiwa kujibu shutuma na madai ya Sheikh Juma Moh’d Al-Mazrui dhidi ya itikadi na imani za Shia Ithna-ashariyya aliyoyaandika katika kitabu chake alichokiita Al-Qistasu Al-Mustaqim (Mezani ya Haki).

Katika kitabu hiki Sheikh Abdilahi Nassir anayajibu yale yaliyoandikwa na Sheikh Al-Mazrui katika Sura ya Tatu na ya Nne ya kitabu chake hicho (uk. 43-114) ya kudai kwamba muradi wa neno ahlul bayt katika Sura 33:33 ni “wake wa Mtume (s.a.w.w.)” si “ahlul-kisaa” kama walivyoshikilia machia na wengi sana wa wanavyuoni wa kisunni.

Ameyajibu hayo kwa kuzijadili kiilimu na kimantiki hujja alizozitegemea Sheikh Al-Mazrui za “sibaaq na siyaaq, kanuni za kiusuli na hujja za kilugha”

 

Common terms and phrases

Bibliographic information