Hadith Al-Thaqalayn: Hadith Sahihi

Front Cover
Ahlul Bayt Centre

Hiki ni kitabu kilichokusudiwa kujibu yaliyochapishwa katika sehemu ya kwanza (uk. 13-42) ya kitabu cha Sheikh Juma Moh’d Al-Mazrui kiitwacho Al-Qistasu al-Mustaqim (Mezani ya Haki).

Katika kitabu hicho, Sheikh Al-Mazrui amejaribu kuthubutisha, kwa hujja alizoona zina nguvu, kwamba ile Hadith ijulikanayo kama Hadith al-Thaqalayn (Hadith ya Vizito Viwili), iliyo mashuhuri sana kwa mashia, si Hadith sahihi; ni “ya kutungwa”!

Katika kitabu hiki, Sheikh Abdilahi Nassir amezijibu hujja hizo zote - moja baada ya moja - kuthubutisha kwamba Hadith hiyo si ya kutungwa bali ni sahihi kabisa - si kwa mashia peke yao, bali hata kwa masunni.

Zaidi ya hayo Sheikh Abdilahi Nassir ameongeza sura moja humu ya kueleza, japo kwa ufupi, historia ya ukusanyaji na uandishi wa Hadithi za Mtume (s.a.w.w.), na jinsi ilivyoathiriwa na siasa na chuki walizokuwa nazo Waislamu, wao kwa wao, katika kipindi cha karne mbili za kwanza baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki dunia. Amefanya hivyo ili kumsaidia msomaji aelewe vizuri kwa nini kumetokea migongano katika kuzitathmini Hadith zake.

 

What people are saying - Write a review

We haven't found any reviews in the usual places.

Bibliographic information